PURA: Tumejaza gesi futi 301.33 miaka minne

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema kwa kipindi cha kuanzia Machi 2021 hadi Machi 2025 kiasi cha gesi kilichozalishwa kimefikia futi za ujazo bilioni 301.33.

Kati ya ujazo huo, futi za ujazo bilioni 142.35 zilizalishwa kutoka kitalu cha Mnazi Bay na futi za ujazo bilioni 158 .98 kutoka kitalu cha Songosongo, Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Charles Sangweni amesema.

Akizungumza katika kikao kazi na wahariri wa habari, kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sangweni amesema kipindi cha nyuma uzalishaji wa nyuma ulikuwa wastani wa futi za ujazo bilioni 32.03 kwa mwaka kwa upande wa Mnazi Bay na futi za ujazo bilioni 25.13 kwa mwaka upande wa Songosongo.

SOMA ZAIDI: PURA kuzifungamanisha sekta za mafuta & gesi na elimu

Aidha, amesema gesi hiyo ilianzishwa ili itumike  kwa matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwandani ,majumbani, taasisi na katika magari.

” Kwa mujibu wa mikataba ya PSA mwekezaji hutumia fedha zake katika utafutaji wa mafuta na gesi asilia ambapo akikosa huwa anarudia eneo kwa serikali na kuondoka lakini pindi akipat mafuta au gesi asilia fedha zinazopatikanazo baada ya mauzo ya rasilimaliwatu iliyopatikana hulipa mrabaha,hurudisha mtaji aliowekeza.

“Hulipa kodi na tozo mbalimbalimbali na kilichobaki hugaiwa kwa wabia wa mkataba ikiwemo serikali na TPDC kwa jinsi hiyo ni muhimu kwa Pura kuhakiki kiasi cha fedha kilichowekezwa pamoja na shughuli zinazotekelezwa ili kuepuka udanganyifu unaoweza kufanywa na mwekezaji, ” amesema Charles.

Naye Mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Tausi Mbowe amesema jukwaa hilo linaahidi kutoa ushirikiano na wao wawape ushirikiano pindi mipango yeyote inayoanza ili kukuza uchumi wa Taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button