Obby Alpha: “Dunia Bila Watu Haina Ladha”

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini, Obby Alpha, amesema kuwa hata mtu akiwa na utajiri au mali nyingi, dunia inaweza kuonekana chungu endapo ataishi peke yake bila kuwa na watu wengine.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Obby Alpha aliandika ujumbe unaosisitiza umuhimu wa watu katika maisha ya kila siku, akieleza kuwa thamani ya vitu tulivyonavyo hutegemea uwepo wa wengine. “Mfano, sisi sote tuondoke duniani tukaacha kila kitu kilichopo leo sidhani kama utaona umuhimu wa chochote pasipokuwa na jirani yako. Dunia haitakuwa na ladha yoyote kama jirani huyo hakuwepo,” alisema.
Mwimbaji huyo aliongeza kuwa baadhi ya watu wanaposhiba au kupata mafanikio, hukumbuka kidogo kuwa wote ni binadamu na wanapaswa kuheshimiana. “Pasipo watu, utu, upendo, amani na ushirikiano dunia si tamu. Watu ndio chumvi ya ulimwengu,” alisema. SOMA: Nyimbo za injili zihubiri maadili



