Mtanzania achomoza ufungaji bora Ufilipino

UFILIPINO; MCHEZAJI wa Tanzania Mary Siyame, yupo kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kiatu cha dhahabu katika fainali za Kombe la Dunia la futsal kwa wanawake zinazoendelea mjini Manila, Ufilipino.

Tanzania ilianza vibaya michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 10-0 na Ureno mchezo wa kwanza, kabla ya kuzinduka jana na kuifunga New Zealand mabao 4-2, huku Mary akifunga mabao matatu.

Mary anawania nafasi hiyo na Emily wa Brazil, Vane Sotelo wa Hispania, Ana Azevedo wa Ureno, Sara Boutimah wa Italia, Sara Oino wa Japan na Derika Peanpailun wa Thailand wenye mabao matatu kila mmoja, huku Renata Adamatti wa Italia akiongoza mbio hizo kwa kupachika mabao manne.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button