NEMC yashiriki mkutano wa UNOC3 Ufaransa

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashiriki mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usimamizi wa Bahari (UNOC3) unaofanyika jijini Nice, Ufaransa kuanzia Juni 9 hadi 13, 2025.

Mkutano huo unaohudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dk Immaculate Sware Semesi ambapo kwa Tanzania umewakilishwa na Makamu wa Rais Dk Philip Isdor Mpango umelenga kujadili na kuhamasisha utekelezaji wa mpango mkakati wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UN-SDG-14).

Kwa mwaka 2025 Mkutano huo umebeba Kaulimbiu, “𝐂𝐡𝐨𝐜𝐡𝐞𝐚 𝐡𝐚𝐭𝐮𝐚 𝐳𝐚 𝐡𝐚𝐫𝐚𝐤𝐚 𝐧𝐚 𝐮𝐬𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐢𝐚𝐧𝐨 𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐝𝐚𝐮 𝐰𝐨𝐭𝐞 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐤𝐮𝐡𝐢𝐟𝐚𝐝𝐡𝐢 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐭𝐮𝐦𝐢𝐳𝐢 𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐯𝐮 𝐲𝐚 𝐁𝐚𝐡𝐚𝐫𝐢” ambayo inalenga kuhamasisha wahusika wote kuhifadhi na kutumia Bahari kwa maendeleo endelevu.

Mkutano huo pia umewakutanisha viongozi wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Kimataifa, Taasisi, Asasi za kiraia pamoja na Sekta binafsi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button