NEMC yashiriki mkutano wa UNOC3 Ufaransa

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashiriki mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usimamizi wa Bahari (UNOC3) unaofanyika jijini Nice, Ufaransa kuanzia Juni 9 hadi 13, 2025.
Mkutano huo unaohudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dk Immaculate Sware Semesi ambapo kwa Tanzania umewakilishwa na Makamu wa Rais Dk Philip Isdor Mpango umelenga kujadili na kuhamasisha utekelezaji wa mpango mkakati wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UN-SDG-14).
Kwa mwaka 2025 Mkutano huo umebeba Kaulimbiu, “๐๐ก๐จ๐๐ก๐๐ ๐ก๐๐ญ๐ฎ๐ ๐ณ๐ ๐ก๐๐ซ๐๐ค๐ ๐ง๐ ๐ฎ๐ฌ๐ก๐ข๐ซ๐ข๐ค๐ข๐๐ง๐จ ๐ฐ๐ ๐ฐ๐๐๐๐ฎ ๐ฐ๐จ๐ญ๐ ๐ค๐๐ญ๐ข๐ค๐ ๐ค๐ฎ๐ก๐ข๐๐๐๐ก๐ข ๐ง๐ ๐ฆ๐๐ญ๐ฎ๐ฆ๐ข๐ณ๐ข ๐๐ง๐๐๐ฅ๐๐ฏ๐ฎ ๐ฒ๐ ๐๐๐ก๐๐ซ๐ข” ambayo inalenga kuhamasisha wahusika wote kuhifadhi na kutumia Bahari kwa maendeleo endelevu.
Mkutano huo pia umewakutanisha viongozi wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Kimataifa, Taasisi, Asasi za kiraia pamoja na Sekta binafsi.