Madeni MSD yalipwe – RC Mwassa

KAGERA: VITUO Vya kutolea huduma za afya vimetakiwa kuhakikisha vinalipa madeni wanayodaiwa na Bohari ya Dawa (MSD) kabla ya mwaka wa fedha 2024/2025 haujaisha.
Akizungumza leo Juni 27, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Mstaafu, Hamis Mahiga amesema ili kujenga huduma madhubuti washirika wanapaswa kulipa madeni yao ili kupata huduma kwa wakati kutoka MSD.
Aidha, RC Mahiga ametoa wito kwa wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Kagera na waganga wakuu wa wilaya na mkoa kuhakikisha wanatumia vyanzo vingine vya mapato kulipa madeni kwa wakati kwani wananchi wanaopata huduma za afya wapate huduma zote muhimu.

Amevitaka vituo vya afya kuhakikisha vinadhibiti mianya inayoweza kupunguza mapato pamoja na watumishi wote kupata uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya kidigitali katika maswala ya kuagiza dawa unaolenga kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
SOMA ZAIDI
Mkurugenzi wa MSD Kanda ya Kagera, Kalendelo Masatu akitoa mwenendo wa huduma kwa wateja amesema serikali umetumia fedha kuhakikisha vituo vinavyopata huduma za MSD vinapokea fedha ambapo Kanda ya Kagera MSD inahudumia Mkoa wa Kagera na Geita katika vituo 413.
Amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni vituo vya afya kudaiwa ambapo Mkoa wa Kagera mpaka sasa unadaiwa zaidi ya Sh bilioni 3.2 na Mkoa wa Geita Sh bilioni 2.2.

Amesema vituo vinapaswa kulipa kwa wakati kwani ucheleweshaji wa fedha na mrundikano wa madeni unaweza kuathiri upatikanaji wa huduma kutoka katika bohari hiyo .
Alibainisha changamoto nyingine kuwa ni baaadhi kushindwa kutumia mfumo wa kidigital katika maswala ya kuagiza mizigo ya dawa,kuagiza dawa bila kuzingatia mahitaji kamili, kutopeleka taaarifa kwa wakati na baadhi kushindwa Kuandika taarifa.
Amesema MSD itaendelea kushirikiana na wadau wote katika kuhakikisha wanapata huduma bora pamoja na kujadili changamoto kwa pamoja Ili kuzitatua kwa msitakabari wa kuhakikisha Kila mwananchi anapata huduma kwa gharama nafuu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera amesema kuwa mkoa huo umepunguza deni kutoka Sh bilioni 6.3 zilizikuwa zinadaiwa na MSD hadi Sh bilioni 3.2 huku akidai kuwa mikakati iliyopo kwa sasa ni kuhakikisha asilimia 50 ya mapato yote ya vituoni inaendelea kulipa deni hilo haraka ili kumaliza deni lote.



