Kiswaga achukua fomu ya kuomba ridhaa ubunge Kalenga

IRINGA: Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga, amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania tena ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesisitiza kuwa bado ana dhamira ya kulitumikia taifa kwa kushirikiana na wananchi wa Kalenga katika kusukuma maendeleo.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kulihutubia Bunge na kutangaza rasmi kulivunja Agosti 3, 2025.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo leo Kiswaga alisema: “Nimekuja kuchukua fomu hii kutii agizo la chama chetu na kuendelea na dhamira yangu ya kulitumikia Jimbo la Kalenga.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano, wana Kalenga wameshuhudia maendeleo makubwa.

CCM yazuia wapambe, misafara uchukuaji fomu

Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia imewaletea fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali, mingine imekamilika na mingine inaendelea kutekelezwa.

Amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana, bado kuna changamoto chache ambazo zinahitaji kushughulikiwa kwa ushirikiano na wananchi, akisisitiza kwamba uzoefu wake katika siasa na utumishi wa umma unampa nguvu mpya ya kukamilisha kazi hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button