Mwanasheria autaka ubunge Muleba Kaskazini

MULEBA: KIONGOZI mwandamizi Chama cha Wanasheria (TLS) Mkoa wa Arusha, Fortunatus Muhalila amechukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea ubunge Muleba Kaskazini.
Muhalila anakuwa miongoni mwa makada anayeheshimaka katika maswala ya mpira wa miguu katika Wilaya ya Muleba hasa baada ya kuanzisha ‘Muhalila Cup’.

Anakuwa miongoni mwa wagombea wengine ambao mpaka sasa wamechukua fomu za kugombea ubunge jimbo hilo.
SOMA ZAIDI
Mwaka 2013 hadi 2018 Muhalila aliwahi kuwa wakili katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amekuwa mushauri kitengo cha Sheria makao makuu CCM Dodoma.

