Wananchi Sinani, Rahaleo kunufaika na mradi wa maji

MTWARA: ZAIDI ya wakazi 1,500 wanaoishi mtaa wa Sinani na Rahaleo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara kunufaika na mradi wa maji uliyogharimu zaidi ya Sh milioni 20.

Hayo yamebainishwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji ujulikanao kama ‘Water for life’ uliyopo mtaa wa Rahaleo kwenye manispaa hiyo, uliyojengwa chini ya Chama cha Wahandisi na Wasanifu Majengo Duniani kupitia Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Sinani, Hawana Libanika amesema uwepo wa mradi huo ni faida kubwa kwa wakazi hao kutokana umeongeza tija ya upatikanaji wa huduma kwa jamii hiyo.

‘’Tunaishukuru taasisi hii ya Ahmadiyya kwa kutuletea huduma hii ambayo itaongeza ufanisi wa upatikanaji wa maji kwenye maeneo yetu na hasa sisi akina mama tunashukuru sana kwasababu tunazidi kupata maji kirahisi na wakati wote,’’amesema Hawana.

SOMA ZAIDI

Mradi wa maji wa bil 12.8/-wazinduliwa Lamadi

Meneja Masoko wa Jumuiya hiyo ya Ahmadiyya mkoani humo, Mwalimu Abdallah Mbanga amesema sekta hiyo imejikita katika maeneo mengi ikiwemo elimu, afya na mengine hivyo wanaangalia fursa ambazo wanaweza kusaidia katika jamii.

Amesema kwa mkoa huo wa mtwara wameona huduma wanayoweza kuitoa kwa jamii hiyo ni maji ambayo yanatolewa bure bila kumbagua mtu.

Naye Sheikh wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya mkoani humo, Shahab Ahmad amesema miradi kama hiyo ikiendelea kuongezeka katika jamii ni imani yake kuwa kero hiyo ya maji itapungua.

Aidha mradi huo umeshatekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mkoani Shinyang, Geita, Tanga, Dar es salaam, Pwani na mingine lakini kwa mkoa huo wa mtwara ndiyo unaanza kutekelezwa hasa katika manispaa hiyo ya mtwara mikindani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button