Misime akitoa wasilisho mkutano wadau wa habari

DAR ES SALAAM: MSEMAJI wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime akitoa wasilisho kwa wadau wa Sekta ya Habari kuhusu wajibu wa Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama wakati wa uchaguzi.
Ametoa wasilisho hilo wakati wa mkutano wa wadau hao kujadili mchango wa sekta ya habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025 ambao umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Julai 9, 2025.



