Tanzania kuandikishwa urithi wa dunia

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amesema wizara hiyo imeanza mchakato wa kuiandikisha Tanzania katika urithi wa dunia usioshikika kwa maana ya nchi inayobeba lugha zote Afrika.

Kabudi amesema hayo leo Julai 9, 2025 katika Mkutano wa Wadau wa Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika Kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025 ambao umefanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Hii kwa sababu ya jitihada zilizofanywa na baada ya uhuru kuunda taifa moja na ndio lilikuwa jukumu kubwa la baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” amesema Kabudi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button