Ulaya Kuijenga Upya Ukraine

ROME: VIONGOZI wa mataifa ya Ulaya wamezindua mkutano wa kila mwaka wa kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ukraine baada ya vita, wakilenga kukusanya zaidi ya Dola za Marekani bilioni 12.
Mkutano huo umefanyika jijini Rome, Italia, na kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni pamoja na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky.Viongozi hao wamewataka wawekezaji binafsi na kampuni kuwekeza katika miradi mbalimbali itakayosaidia mpango wa ujenzi wa Ukraine, hususan katika sekta ya miundombinu, nishati, na huduma za kijamii. SOMA: Marekani, Ulaya, Ukraine kujadili mzozo wa Urusi
Mkutano huo umefanyika wakati ambapo Urusi inaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Ukraine, huku ripoti ya Umoja wa Mataifa ikionya kuwa idadi ya wahanga wa vita hivyo imefikia kiwango cha juu zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na waandaaji wa mkutano huo, fedha zitakazopatikana zitaelekezwa katika kusaidia waathirika wa vita, ujenzi wa shule, hospitali, pamoja na mifumo ya usambazaji maji na umeme.