Dk Mpango afungua mkutano wa waganga wakuu

DODOMA: Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango leo Julai 12, 2025 amefungua rasmi Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri jijini Dodoma.
Dk Mpango ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi Rais- TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama.
Mkutano huo wa siku tatu umeanza jana na unatarajiwa kumalizika hapo kesho.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni“Wajibu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika kuimarisha ubora wa huduma za afya kuelekea bima ya afya kwa wote”



