Wafungwa kupiga kura Oktoba

DAR-ES-SALAAM : MSIMAMIZI Msaidizi wa Jimbo la Kivule, Wilaya ya Ilala, Dk. Mussa Ally ameipongeza serikali kwa kuwaruhusu wafungwa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu kwa mara ya kwanza.

Akizungumza na Daily News Digital, Dk. Mussa amesema hatua hiyo ni miongoni mwa maboresho makubwa kuelekea uchaguzi huo, ikiwemo kuhakikisha kila Mtanzania anatimiza haki yake ya kikatiba. “Tumefarijika kuona serikali imewaruhusu wafungwa kupiga kura, hii itakuwa mara ya kwanza,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Mussa, uamuzi huo unaonyesha dhamira ya serikali kuhakikisha ushirikishwaji wa makundi yote katika mchakato wa kidemokrasia nchini. SOMA: Bodi ya Parole yaridhia msamaha wa wafungwa

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button