Bodi ya Parole yaridhia msamaha wa wafungwa

ARUSHA: BODI ya Parole Taifa imeridhia wafungwa 118 kati ya 132 kunufaika msamaha wa vifungo kutokana na makosa mbalimbali waliyokutwa nayo huku wafungwa 14 wakishindwa kukidhi vigezo.

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Balozi Khamis Kagasheki wakati kikao cha bodi cha 52 kilichoketi Arusha kwa siku mbili.

Amesema wafungwa hao wanaostahili kunufaika na utaratibu wa parole ni wale walitumia kifungo chao kwa muda fulani kama sheria inavyotaka.

SOMA ZAIDI: Kikongwe agoma kupokea msamaha wa Rais Trump

“Kikao hiki kimepitia mashauri 132 ambapo mashauri 118 ya wafungwa ndio yametolewa maamuzi ya kunufaika na msamaha lakini huu ni uamuzi wa bodi na waziri mwenye dhamana hii ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani atapelekewa kwa aajili ya maamuzi ”

Amesema katika kikao hicho mashauri 14 waliyoyapitia kati ya 132 yalionekana kutodhi vigezo vigezo hivyo bodi hiyo iliona wafungwa 118 pekee ndio wanastahili kukidhi vigezo husika.

Naye Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) Jeremiah Katungu amesema kazi kubwa ni kujadili mapendekezo ya parole yaliyowasilishwa kuanzia ngazi ya chini hadi taifa hiku vigezo vinavyotokana na nidhamu njema, huku akisisitiza utaratibu wa parole umekuwa na mafanikio makubwa ndani ya jeshi la magereza pamoja na taifa kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button