CCM yawaonya wanaohamasisha uvunjifu wa amani

DODOMA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, za kuharakisha maendeleo ya wananchi huku kikisisitiza kuwa amani, umoja na mshikamano ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Juni 13,2026 Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amesema chama hicho kimeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanywa na serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, maji, umeme, barabara, kilimo na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.

Amesema katika ziara za chama zilizofanyika katika mikoa 12 na wilaya 41, viongozi wa CCM wamejionea mafanikio makubwa yaliyopatikana pamoja na kusikiliza changamoto za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi kupitia serikali.
βTumeshuhudia kazi kubwa inayofanywa na serikali ya CCM chini ya Rais Samia. Fedha nyingi zimepelekwa katika miradi ya maendeleo na wananchi wanaendelea kunufaika na maboresho ya huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali nchini,β amesema.

Kihongosi amesema pamoja na mafanikio hayo, baadhi ya changamoto zilizobainika ni migogoro ya ardhi, huduma ya maji katika maeneo machache na vitongoji ambavyo bado havijafikiwa kikamilifu na huduma ya umeme, huku akieleza kuwa serikali inaendelea kuzitatua kupitia bajeti na miradi inayoendelea kutekelezwa.
Amesema maendeleo ya taifa hayawezi kupatikana kwa siku moja bali yanahitaji muda, mipango na uwekezaji endelevu, akibainisha kuwa Tanzania ya sasa imepiga hatua kubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa miaka mitano au 10 iliyopita.
Aidha, amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kufungua fursa za kiuchumi kupitia diplomasia ya kimataifa, hatua ambayo imeongeza uwekezaji na ushirikiano wa maendeleo kwa manufaa ya taifa.
Kuhusu Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/27 ya zaidi ya Sh trilioni 62, Kihongosi alisema bajeti hiyo itaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha huduma muhimu kwa wananchi, huku akisisitiza kuwa ni ushahidi wa dhamira ya serikali ya kuendelea kuwaletea maendeleo Watanzania.




Uanzishwaji wa taasisi Maeneo ya Mapinga kwa ajili ya uzalishaji wa mchele wa nazi unaleta mageuzi ya viwanda na kilimo. Hatua hii itagusana moja kwa moja na Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 2022, Sheria ya Mazao na Nafaka (COPRA), pamoja na sheria za mazingira NEMC na TFDA kwa ajili ya usalama wa chakula.Zifuatazo ni sheria zitakazoathirika na taratibu zake maalum:
1. Sheria za Kilimo na Udhibiti wa Mazao (COPRA)
Sheria Husika: The Cereals and Other Produce Act inayosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA).
Athari: Uzalishaji wa mchele wa nazi (kuchanganya nazi na mchele kupata bidhaa mpya) utahitaji usajili wa kiwanda, vibali vya viwango vya ubora, na ukaguzi wa mara kwa mara kutoka COPRA.2.
Sheria za Uwekezaji na ArdhiSheria Husika:
Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Na. 10 ya 2022 na Sheria ya Ardhi (Sura ya 113).
Athari: Taasisi itapaswa kujisajili kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kupata hati ya vivutio (Investment Certificate) na kuomba matumizi sahihi ya ardhi katika eneo la Mapinga kupitia mabaraza ya ardhi ya wilaya.
3. Sheria za Mazingira na Vibali vya Ujenzi (NEMC)
Sheria Husika: Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (Sura ya 191) inayosimamiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Athari: Kabla ya kuanza ujenzi wa kiwanda Mapinga, taasisi italazimika kufanya tathmini ya athari kwa mazingira (EIA) na kupata cheti cha mazingira.
4. Sheria za Viwango na Usalama wa Chakula
Sheria Husika: Sheria ya Mamlaka ya Dawa, Vifaa Tiba na Chakula (TMDA) au TBS.
Athari: Bidhaa ya mchele wa nazi lazima ifanyiwe utafiti wa kimaabara, ithibitishwe usalama wake kwa mlaji, na kupewa alama ya ubora kabla ya kuanza kuuzwa sokoni au kusafirishwa.
β 彑[ππππ ππππππ π ππ ππππ ππππ ππππππ ππππ]彑β
I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $35,000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my lifeβ¦ This is what I do, check it out by visiting Following Linkβ¦
.
You can check moreβ¦β¦β¦β¦β¦β¦ https://Www.Payathome9.Com