CCM kufanya mkutano mkuu maalumu kesho

DODOMA: CHAMA Cha Mapinduzi ( CCM ) kimesema kesho Julai 26, 2025 kitafanya Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama hicho kwa njia ya mtandao.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama hicho, Amos Makalla amesema lengo kuu la mkutano huo ni marekebisho madogo ya Katiba ya CCM.

Makalla amesema mkutano huo utakaofanyika jijini Dodoma, utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button