Maonesho ujuzi, ajira yadhihirisha uwekezaji wa Uswis kwa vijana TZ

IRINGA: Naibu Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Nicole Providoli, ameshiriki uzinduzi wa maonyesho ya ujuzi, fani na ajira kwa vijana mjini Iringa, akiipongeza jamii ya Iringa kwa ukarimu na dhamira ya kweli katika kuliwezesha kundi hilo kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

Amesema kati ya mwaka 2022 na 2025, serikali ya Uswisi imewekeza zaidi ya Sh Bilioni 23 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupitia mradi wa Skills for Employment Tanzania (SET) unaotekelezwa na taasisi ya Swisscontact, ikiwa ni sehemu ya kusaidia nguvu kazi ya taifa kwa kuwapatia maarifa, ujuzi na fursa za kazi.

“Tumefika Iringa tukiamini kuna fursa kubwa kwa vijana. Tunaona ni wakati sahihi kusaidia vijana waliomaliza shule na vyuo kutafsiri maisha kulingana na elimu waliyonayo na mahitaji ya ajira yaliyopo mtaani,” alisema Balozi Providoli.

Alisema wakiwa ni washirika wa maendeleo wa Tanzania wataendelea kufadhili mahitaji ya vijana ili kuwajengea uwezo wa kweli wa maisha na uchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Swisscontact nchini Tanzania, Rudolf Nuetzi, alisema maonyesho hayo ni jukwaa muhimu la kuwaleta pamoja waajiri, watoa mafunzo, taasisi za kifedha, serikali na vijana kwa ajili ya kujenga mfumo shirikishi wa maendeleo ya ajira na ujasiriamali.
Alieleza kuwa mradi wa SET umebadilisha maisha ya maelfu ya vijana nchini na kutoa mfano wa kijana kutoka Morogoro aliyekosa mwelekeo lakini kupitia programu hiyo sasa ameweza kuanzisha biashara na kuwaajiri vijana wengine wawili.

“Ni wakati wa vijana wa Iringa kuamsha fikra na kushinda changamoto zao kwa vitendo,” alisisitiza.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Astomini Kyando, alisema maonesho hayo si tu yanatoa elimu bali yanajenga fursa za maisha, ujasiriamali, mitandao ya kikazi na ushirikiano na taasisi mbalimbali.

“Maonesho haya ni mkombozi kwa vijana wetu. Yamewasaidia kuelewa ujuzi unaohitajika sokoni, kukutana na waajiri, wajasiriamali waliobobea, na taasisi za kifedha kwa ajili ya msaada wa mitaji. Tunawashukuru wadau wetu wa Uswisi kwa kuona thamani ya vijana wetu,” alisema DC Kyando.

“Niwashukuru Ubalozi wa Uswisi kwa kuendelea kuwa washirika wa kweli wa maendeleo. Mmechangia moja kwa moja utekelezaji wa sera zetu na maendeleo ya viwanda. Tunaikaribisha Swisscontact kuendelea kuwekeza katika sekta ya ujuzi hapa Iringa,” alisema.

Maonesho haya yaliyoandaliwa na Swisscontact kupitia mradi wa SET na kufadhiliwa na Ubalozi wa Uswisi, yamewakutanisha zaidi ya washirika 50 kutoka sekta ya umma, binafsi, NGOs, taasisi za mafunzo ya ujuzi na taasisi za kifedha.

Hadi sasa, zaidi ya vijana 3,000 wamehudhuria maonesho hayo ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo:
“Kijana: Ujuzi Wako, Fani Yako, Chaguo Lako.”

Habari Zifananazo

22 Comments

  1. ‘His cognitive deficits significantly impair his ability to understand the nature
    and consequences of the charges, consult with counsel in a rational manner, and
    participate in his defense “with a reasonable degree of rational understanding,” the.

  2. With havin so much content and articles do you ever run into any
    issues of plagorism or copyright infringement? My
    blog has a lot of exclusive content I’ve either created myself or outsourced but it appears a lot of it is popping it up all over
    the intetnet wighout my agreement. Do you know
    any methods to help stop content from being ripped off?

    I’d really appreciate it.

  3. ‘Our results suggest that vitamin D deficiency may contribute
    to the lack of response to this first-line treatment of
    erectile dysfunction’, said Dr Miguel Olivencia, a researcher at Complutense University
    and co-author of the study. 

  4. I’ve been exploring for a little bit for any high quality articles or
    weblog posts in this kind of house . Exploring in Yahoo
    I ultimately stumbled upon this website. Studyinng this info So i’m glad to exhibit that I’ve an incredibly just right uncanny feeling I found out exactly what I needed.

    I so much unquestionably will make sure to don?t put
    out of your mind this site and give it a glance regularly.

    my site … buy Closet Carousel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button