Biashara ya binadamu yaongezeka-IOM

ASIA : UMOJA wa Mataifa kupitia Shirika lake la Uhamiaji (IOM), umesema biashara haramu ya binadamu inaendelea kuongezeka kwa kasi ya kutisha, huku maelfu ya watu wakikumbwa na udanganyifu wa mitandaoni katika eneo la Kusini-Mashariki mwa Asia.
Taarifa hiyo imetolewa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadamu, ambapo IOM imeeleza kuwa waathirika wengi wa biashara hiyo hukamatwa kwa tuhuma ambazo hawajazifanya, badala ya kusaidiwa.
Mkurugenzi Mkuu wa IOM, Amy Pope, amesema biashara hiyo si tu kwamba ni tishio kwa haki za binadamu, bali pia ni chanzo kikuu cha ufisadi na hofu duniani, huku ikitajwa kuingiza wastani wa dola bilioni 40 kila mwaka. “Waathirika wakubwa ni wahamiaji, vijana wanaotafuta ajira, watoto na watu wenye ulemavu,” amesema Bi. Pope.
Amezitaka serikali na mashirika ya kiraia duniani kushirikiana katika kubadili sheria za kitaifa ili kulinda waathirika na kuhakikisha hawadhibiwi kwa uhalifu usiotokana na wao. SOMA: Biashara ya binadamu ipo-Chalamila