Ursula,Zelensky kuungana Marekani

 WASHINGTON DC : VIONGOZI wa mataifa ya Ulaya wanatarajiwa kuungana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine leo Jumatatu nchini Marekani kwa mazungumzo na Rais Donald Trump kuhusu namna ya kumaliza vita vya Ukraine.

Mkutano huo unafuatia mazungumzo ya Trump na Rais Vladimir Putin wa Urusi yaliyofanyika Ijumaa, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kumaliza vita Ukraine.Kwa mujibu wa taarifa, ajenda kuu ni kujadili mapendekezo ya amani ambayo yanajumuisha Ukraine kuachia baadhi ya maeneo yake.

Viongozi wanaotarajiwa kushiriki ni Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni. SOMA: Trump, Putin kukutana Alaska wiki hii

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button