Mazoezi ya kijeshi yaiva Seoul

SEOUL : KOREA KUSINI kwa kushirikiana na Marekani wameanza mazoezi makubwa ya kijeshi ya pamoja yanayolenga kukabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini.

Mazoezi hayo yanatarajiwa kudumu kwa siku 11, huku mazoezi mengine makubwa zaidi yakipangwa kufanyika mwezi Machi mwakani. Korea Kaskazini imeonya kuwa hatua hiyo itazidisha mivutano ya kikanda na imeapa kujibu kwa nguvu iwapo kutakuwa na uchokozi wowote dhidi yake.

Luteka hiyo ya kila mwaka, ambayo hufanyika Korea Kusini, imeanza wakati Rais mpya wa Korea Kusini, Lee Jae Myung, akijiandaa kufanya mkutano wake wa kwanza na Rais wa Marekani, Donald Trump, ifikapo Agosti 25. SOMA: KOREA KUSINI : Rais Yoon Suk avunja ukimya

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button