Simba, Yanga kupigwa Septemba 16

DAR ES SALAAM: Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) ya kuizindua msimu mpya wa Ligi Kuu kati ya Young Africans na Simba itachezwa Septemba 16, 2025 jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa TFF, Mfumo wa mashindano ya Ngao ya Jamii umebadilika kutokana na marekebisho ya kanuni yaliyopitishwa katika kikao kilichopita cha Kamati ya Utendaji ya TFF.



