TASAF sasa hadi 2025

RAIS  Samia Suluhu Hassan ameongeza muda kwa  wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF) hadi mwaka 2025.

Hayo yamesemwa na NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi wakati akizungumza na wanufaika wa mradi huo Kata ya Rusimbi iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji mkoani Kigoma.

Amesema Rais Samia kwa mapenzi aliyonayo kwa watanzania ameamua kuuongezea muda mradi huo hadi mwaka 2025 ambapo awali mradi huo ulikua uishe mwaka 2023.

” Nimpongeze na nimshukuru Rais Samia kwa upendo aliouonesha wa kutuongezea muda wa mradi huu na sasa utaenda hadi mwaka 2025 badala ya mwaka 2023 ambapo ungemalizika. Hili ni jambo kubwa ambalo Hakika Rais wetu amelifanya kwa wanufaika wa TASAF.”Amesema

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button