Mtoko wa Yanga ni kesho

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imetangaza kuzindua jezi rasmi zitakazotumika kwenye michezo ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26. Uzinduzi huo utafanyika saa 6 mchana kesho.
Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ali Kamwe ametoa taarifa hiyo leo alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
“Tutakuwa na namna ya kipekee ya kuzindua mtoko wetu, hii ni namna ambayo itawashangaza, itawafurahisha na itawafikirisha kwenye kile sisi tunachokiwaza kuhusu biashara,” amesema Ali Kamwe.



