MOF yakabidhi mil 1/- kwa wenye uhitaji Temeke

DAR ES SALAAM: FEDHA kiasi cha milioni 1/- kimekabidhiwa kwa kituo cha kulea watoto wenye uhitaji cha Jeshi la Wokovu kilichopo maeneo ya Uhasibu, Temeke Dar es Salaam.
Kiasi hicho kimekabidhiwa kutoka kwa Taasisi ya Miriam Odemba Foundation ikiwa ni muendelezo wa taasisi hiyo kurudisha kwa jamii na kusaidia wenye uhitaji.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Miriam Odemba amesema hatua hiyo muhimu ni katika kuthamini jamii iliyomzunguka kwa kutambua kuwa ipo haja ya kuendelea kuwaunga mkono watoto wenye uhitaji.
SOMA ZAIDI
Miriam amesema imekuwa kawaida kwa taasisi yake kufanya hivyo, kwani kwa miaka mingi amekuwa akirudisha kwa jamii.
“Taasisi zipo nyingi, ila upekee wa Miriam Odemba Foundation unajulikana, tunasaidia maeneo mengi sana, shuleni, taasisi za dini, vituo vya yatima, tutaendelea kufanya hivyo,” amesema Miriam.
Hatua hiyo inakuja baada ya miezi kadhaa taasisi hiyo kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutoa misaada mbalimbali na kuwajulia hali wagongwa.