Taasisi ya Miriam Odemba kufanya kampeni uchangiaji damu

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Miriam Odemba Foundation (MOF) inakusudia kufanya kampeni ya kuchangia damu, kutembelea wodi za wazazi na kutoa huduma zingine za afya Julai 25, jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya taasisi hiyo imeeleza kuwa lengo ni kusaidia wamama na kuchangia kwa namna tofauti kuwapa huduma za afya.
Taasisi hiyo pia imewakaribisha wadau wa afya na wale wataoguswa kwa namna tofauti kushiriki zoezi hilo sambamba na kutoa michango yao kukamilisha zoezi hilo.
Miriam Odemba Foundation ni taasisi inayomilikiwa na Mwanamitindo Mtanzania mwenye makazi yake nchini Hispania, Ufaransa na Uswis Miriam Odemba.
Aidha, kupitia taasisi yake imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kuwezesha wanafunzi wa kike taulo za hedhi, ujenzi wa vyoo vya shule mbalimbali na kusaidia wenye uhitaji.