Majaliwa alipongeza soko la hisa Dar

DAR ES SALAAM: WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amelipongeza Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kuongezeka kwa thamani ya soko hilo na kufikia Sh trilioni 21.0 katika kipindi cha kufikia Julai 2025.

Amesema pia soko hilo limeongeza ukuaji wa mauzo ya hisa kwa zaidi ya asilimia 246 pamoja na ongezeko la idadi ya wawekezaji hadi zaidi ya akaunti 683,000 ikiwa ni ishara ya ukuaji imara wa sekta ya mitaji nchini.

Amesema hayo leo Agosti 26, 2025 alipotembelea ofisi za soko hilo zilizopo Morocco, jijini Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button