Kishindo cha kampeni CCM

DAR ES SALAAM: MIONGONI mwa majukumu kubwa la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kueleza mafanikio ya Ilani 2020/2025, lakini pia kuwapa wananchi majawabu ya Ilani mpya kuelekea Uchaguzi Mkuu ukaofanyika Oktoba mwaka huu, ambapo dirisha la kampeni linafunguliwa kesho Agosti 28 saa 12 asubuhi.

Aidha, CCM imeahidi kufanya kampeni hizo kwa amani, ustaarabu, tija na kulinda heshima ya nchi bila kudhalilisha utu wa yoyote huku chama hicho kikidai kuwa kimejijenga katika misingi inayotambua binadamu wote ni sawa.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Agosti 27, 2025, kuhusu ushiriki wa chama hicho kwenye kampeni hizo, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi amesema kazi nyingine ya chama hicho itakuwa kunadi wabunge katika majimbo 12 ya Mkoa wa Dar es Salaam na madiwani.

“Hivyo tutumie nafasi hii kuwakaribisha Wajumbe wa Kamati Kuu wote, wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa, lakini Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM, viongozi wa dini, na wanachama wote wa Dar es Salaam na viongozi wa chama wa mikoa yote,” amesema Kihongosi.

Akizungumzia Ilani mpya ya 2025/2030, Kihongosi amesema ni Ilani bora iliyobeba matumaini katika sekta zote zinazowagusa wananchi, sio hivyo tu amesema CCM imebeba wagombea bora wenye uwezo na uzoefu ndani ya chama hicho na serikali pia.

“Ukichukuwa wasifu wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Samia Suluhu Hassan utaona umesheheni mambo mengi makubwa, lakini wasifu wa mgombea mwenza, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi utaona umesheheni uzoefu wa kutosha, hivyo CCM imeleta wagombea waliobeba matarajio ya kutatua changamoto za wa watanzania,” ameeleza Kihongosi.

SOMA ZAIDI

“Epukeni kampeni za matusi”

Aidha, kwa mujibu wa tangazo la Julai 26, 2025 lililotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 28, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Bara. Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 27, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa Zanzibar.

Kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na madiwani kwa Tanzania Bara jumla ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Aidha, kwa upande wa Zanzibar, wapiga kura 725,876 wapo katika Daftari la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na wapiga kura 278,751 wameandikishwa na INEC kwa kuwa hawakuwa na sifa za kuandikishwa na ZEC.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button