Queen Lugembe arejesha fomu ya ubunge Ubungo

DAR ES SALAAM: MWANAHARAKATI na kada wa chama cha ACT-Wazalendo, Queen Julieth Lugembe, leo amerejesha rasmi fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia chama hicho, hatua inayomwezesha kupeperusha bendera ya ACT-Wazalendo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi wa chama, wanachama na wafuasi wake, Queen Julieth alisisitiza dhamira yake ya kuwatumikia wananchi wa Ubungo kwa uwazi, uwajibikaji na mshikamano wa kweli.
“Dira yangu ni kuhakikisha sauti za wananchi zinapata nafasi bungeni. Niko tayari kusimama na watu wa Ubungo ili tuweze kujenga maendeleo yenye usawa na mshikamano,” alisema Lugembe mara baada ya kurejesha fomu hiyo.
SOMA ZAIDI
Wananchi na mashabiki wa chama hicho walijitokeza kwa wingi kumpokea, wakimpongeza na kumtakia kila la heri katika safari yake ya kisiasa, huku wakionesha imani kuwa anaweza kuleta mabadiliko katika jimbo hilo.
Kwa kurejesha fomu hiyo, Queen Julieth sasa anasubiri mchakato wa mwisho kabla ya kuanza rasmi kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
I make $88 an hour to work part time on a laptop. I never thought it was possible but my closest friend easily made $18,000 in 3 weeks with this top offer and she delighted me to join. .Visit the following article for new information on how to access…….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com