Balozi Nchimbi: Ushindi unakuja

MWANZA: MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho kinatarajia kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, kwa kuwa wananchi wanahitaji viongozi bora wanaojali maslahi yao kama waliopo kwenye chama hicho.

Nchimbi aliyasema hayo juzi jioni wakati akihutubia umati wa watu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza juzi jioni.

Alisema mapokezi makubwa aliyoyapata tangu alipowasili yameonesha hamasa ya wananchi na uthibitisho kwamba CCM itaibuka na ushindi wa kishindo.

“Wananchi wameniambia Rais Samia Suluhu Hassan alale usingizi kwa sababu mchezo umeisha, ushindi ni wa CCM,” alisema huku akishangiliwa kwa shangwe na mamia ya wananchi.

Alisisitiza kuwa Mgombea Urais wa CCM, Rais Samia ametekeleza ahadi zake kwa bidii na dhamira kubwa ya kuendeleza amani, uhuru na maendeleo ya nchi.

“Tangu alipoapishwa, Samia aliahidi kulinda amani na uhuru wa Tanzania na amefanya hivyo kwa nguvu kubwa. Hili ndilo linawapa wananchi imani kwamba CCM ndiyo chama cha kuaminiwa kuendelea kuongoza taifa,” alisema.

Aidha, Nchimbi alisema dalili za ushindi wa kishindo zimeanza kuonekana kupitia matokeo ya awali ya wagombea wa CCM kupata ushindi mkubwa wa nafasi za udiwani na ubunge jijini Mwanza.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button