Dk Kijaji asema CCM itashinda

DODOMA : MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kondoa mkoani Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Ashatu Kijaji amesema hana mashaka na ushindi wa chama hicho katika uchaguzi mkuu, kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwa kushirikiana na serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta mbalimbali tangu aingie madarakani.
Dk Kijaji alisema hayo juzi baada ya kurejesha fomu ya uteuzi wa kugombea ubunge katika Jimbo la Kondoa kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), mkoani Dodoma. SOMA: Dk Ashatu Kijaji asisitiza uwajibikaji TBS
Akizungumza baada ya kurejesha fomu, alisema ana imani kuwa INEC itatekeleza wajibu wake kwa haki na uwazi. Aidha, Dk Kijaji aliwashukuru viongozi wa juu wa CCM pamoja na wanachama wa chama hicho kwa imani waliyoionesha kwake kwa mara nyingine, akisema yupo tayari kurejea tena bungeni kuendeleza kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Kondoa.



