Dk.Mwinyi: Umoja ndiyo nguvu ya CCM

ZANZIBAR : MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa wanachama wa CCM kudumisha mshikamano na umoja kuelekea Uchaguzi Mkuu wa  mwezi Oktoba, 2025.

Dk. Mwinyi, ambaye pia ni Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya CCM, alitoa kauli hiyo leo alipokutana na waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi Chama Cha Mapinduzi ikiwemo Udiwani, Uwakilishi, Ubunge  wa Majimbo na Viti maalum kwa makundi mbalimbali katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi .

Amesema mshikamano ndani ya chama ni nguzo kuu ya ushindi wa CCM, akiwataka wanachama kuweka mbele maslahi ya chama kuliko maslahi binafsi ili kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi mkubwa. “Tunapaswa kuungana na kushirikiana kwa dhati, ili kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kushika dola na kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,” alisema Dk. Mwinyi. SOMA: CCM Iringa  kumekucha mikutano ya hadhara

 

Habari Zifananazo

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button