Simba Day raha mara mbili!

DAR ES SALAAM; USIKU huu timu ya Simba imehitimisha tamasha lake la Simba Day kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya na kuibuka na ushindi  wa mabao 2-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba iliweka kambi nchini Misri karibu mwezi mmoja kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2025/26, hivyo mchezo wa leo ilikuwa fursa kwa mashabiki kuona wachezaji wapya waliosajiliwa kwa msimu huo.

Licha ya mashabiki wa Simba kupata furaha ya mpira, lakini tamasha la leo pia lilikuwa na burudani mbalimbali za wasanii tofauti, ambao waliwapa raha mashabiki waliohudhuria na wale waliokuwa wakifuatilia kwenye televisheni.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button