IGP mstaafu Mahita atimiza umri wa miaka 80

MOROGORO; MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita (kulia), akiwa na Diwani wa Kata ya Kariakoo Dar es Salaam na msemaji wa zamani wa klabu za Simba na Yanga, Haji Manara, wakati wa dua maalumu na futari ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya IGP Mahita, ambaye ametimiza umri wa miaka 80.
Tukio hilo ambalo Haji Manara pia alikuwa ndiye mwendeshaji wa shughuli lilifanyika jana mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo IGP Mstaafu, Said Mwema. (Picha kwa hisani ya Haji Manara).


