Kolabo ya Amawele yarejea kwa kishindo

DAR ES SALAAM : WIMBO maarufu Amawele uliorekodiwa na wasanii Marioo, Tyla na Ch’cco mnamo Desemba 9, 2022 kupitia albamu ya kwanza ya Marioo The Kid You Know, umeibua mjadala mpya kwenye mitandao ya kijamii licha ya kuwa umetolewa karibu miaka mitatu iliyopita.

Mashabiki wengi nchini wameanza kuuzungumzia upya wimbo huo, hali iliyochangia mkanganyiko kwamba huenda aliyehusika kwenye kolabo hiyo ni msanii Tyler ICU badala ya Tyla. Umaarufu wa Tyla duniani umeongezeka kwa kasi katika kipindi cha hivi karibuni, hasa baada ya wimbo wake Water kufikisha zaidi ya bilioni moja za kusikilizwa mtandaoni (streams) na albamu yake ya kwanza pia kufanikisha rekodi hiyo kwenye Spotify.

Hali hiyo imeibua maswali miongoni mwa mashabiki kuhusu kwa nini Marioo hakuipa msukumo mkubwa kolabo hiyo ya Amawele wakati wa kutoka kwake. SOMA: Chino, Marioo mbona fresh tu! Kwa upande wa Marioo, albamu The Kid You Know ilipata mafanikio makubwa mwaka 2022, huku Amawele pekee ikifikisha zaidi ya milioni 2.4 za streams kwenye Spotify. Hadi sasa, Marioo anaendelea kushikilia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania akiwa na zaidi ya wasikilizaji 450,000 kila mwezi kwenye Spotify.

Mjadala huu umeibua hoja pana kwamba mashabiki wa muziki nchini bado hawana utamaduni wa kusikiliza albamu kwa ukamilifu, badala yake huzingatia nyimbo zinazopandishwa hadhi kama singles au zile zinazopata umaarufu kupitia redio na mitandao ya kijamii. Mfano wa Amawele unaonesha wazi kuwa muziki hauishi siku ya kutolewa pekee, bali thamani yake huongezeka kadri muda unavyosonga na umaarufu wa wasanii husika unavyokua.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button