ACT Wazalendo kuruhusu karafuu iuzwe popote

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman amesema serikali yake itaruhusu wakulima wa karafuu wauze zao hilo popote wanapotaka.

Othman amesema hayo Chokocho, Wilaya ya Mkoani Pemba katika kampeni za chama hicho wa ajili ya Uchaguzi Mkuu.

Amesema serikali yake haitodhibiti zao la karafuu na kuwalazimisha wakulima kuuza karafuu kupitia Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC).

Othman amesema Serikali ya ACT Wazalendo itaweka utaratibu utakaotokana na mipango na mifumo ambayo mkulima atakapouza karafuu zake serikali inapata kodi.

‘’Tukiingia madarakani tunakusudia kufanya mageuzi makubwa ya kilimo cha karafuu ikiwemo kuweka soko huria ambapo kila mkulima yupo huru kuuza karafuu sehemu anayoipenda yeye yenye maslahi tofauti na sasa,’’ amesema.

SOMA: ACT Wazalendo yaahidi serikali jumuishi Z’bar, mshahara mil 1/-

Aidha, Othman amesema anakusudia kutoa mikopo nafuu kwa wakulima wa karafuu kwa ajili ya kuimarisha mashamba na kuotesha miche mipya ili kuchukuwa nafasi ya miche iliyozeeka ambayo haina uzalishaji mzuri.

Kwa mfano amedai kilimo cha karafuu kimeshuka kwa sababu wakulima wanashindwa kuendeleza mashamba kwa kuotesha mikarafuu mipya.

‘’Tumegundua uzalishaji umeshuka kwa sababu wakulima hawana uwezo wa kuendeleza mashamba ya karafuu ambayo baadhi yame mikarafuu iliopo imezeeka sana,’’ amesema Othman.

Awali Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Ismail Jusa Ladhu alisema chama hicho kimejipanga kuharakisha maendeleo ya wananchi.

‘’Wananchi wa Pemba tunawaomba ifikapo Oktoba 29 kura zote za ndiyo kwa mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo,Othman Masoud Othman ambaye amejipanga na kuja na mikakati mingi ya mageuzi ya kiuchumi kwa masilahi ya wananchi wa Zanzibar,’’ amesema Jusa.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Ultimately, I was able to recover $48,500 of my initial deposit, a result I had almost abandoned hope of achieving. My experience served as a valuable lesson. The crypto gaming sector is fraught with hidden dangers, and not every platform is as trustworthy as it presents itself to be. Thorough research is essential, and seeking support from DUNE NECTAR WEB EXPERT is advisable if you encounter Cryptocurrency Fraud.

    – Te/eGram – @dunenectarwebexpert

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button