CCM haisemi kutoka ndotoni-Samia

MGOMBEA wa urais kupitia Chama cha Mpinduzi(CCM), Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi za kuchochea maendeleo ya Jimbo la Mchinga atakazozitekeleza kwa kasi ilele ya miaka mitano iliyopia huku akisisitiza kuwa CCM haisemi kutoka ndotoni.
Akizungumza na umati wa wananchi katika Jimbo la Mchinga, Samia alisema alizibainisha ahadi hizo ni utekelezaji wa miradi ya maji, ikiwamo kuchimba visima itakayohakikisha vijiji 10 vinapata huduma ya majisafi na salama na kuwa lengo ni kuona kila mwananchi ananufaika na majisafi na salama.
Kwa upande wa kilimo, Samia aliahidi kuendelea kutoa ruzuku za pembejeo sambamba kutoa viwatilifu vya sulphur na dawa bure kwa wakulima wa korosho. “Tunafanya hivyo ili kujenga uweze wa wakulima wa Tanzania, tungemtaka mkulima afanye kila kitu mazao yanayopatikana sasa yasingepatikana , mashamba yasingekuwa yanapewa huduma inavyotakiwa, hivyo tunatoa ruzuku ili wakulima wazalisha wauze na kupata fedha, huko mbele tutaangalia msimame kwa miguu yenu, lakini kwa sasa tutaendelea kutoa ruzuku.”
Samia pia aliahidi kuendelea kutafuta masoko yenye bei kubwa na kuwa serikali imetoa Sh bilioni 30.3 kwa ajili ya kutekeleza miradi miwili ya umewagiliaji maeneo ya Lutamba na Kilangala ili wakulima walime mara mbili kwa mwaka. Samia alisema serikali itaendelea kusimamia sekta ya kilimo kwa sababu Tanzania inazalisha mazao kwa wingi hivyo muhimu kuwepo upatikanaji masoko yenye uhakika.
Aidha, Samia alisema kutokana na wakulima kuzalisha sana, aliahidi kujenga soko la kisasa la mazao na likiwa na huduma za mazao ya mboga mboga ambayo pia yana soko nchi za nje. Pia aliahidi kuendelea na ruzuku kwenye chanjo ya mifugo ambapo kwenye ng’ombe serikali imekuwa ikibeba nusu ya gharama wakati kwenye chanjo ya kuku itaendelea kutolewa bure.
Samia pia alisema mbali na chanjo serikali itakwenda kujenga majosho na machinjio bora kwa mifugo ili nyama ya Tanzania iwe yenye viwango kutambulika maeneo mbalimbali duniani. Kwa upande wa uvuvi, Samia alisema serikali ilitoa mikopo ya boti za kisasa za uvuvi zenye thamani ya Sh milioni 712 huku awamu ijayo serikali itaendelea kutoa boti na vifaa vya uvuvi.
Pia, alibainisha katika maeneo ya Mkoa wa Lindi huduma zote za afya zinapatikana zikiwemo za kibingwa baada ya uwepo wa hospitali kubwa ya rufaa. Kuhusu elimu, Samia alisema endapo akipewa ridhaa ya kuliongoza taifa, serikali yake itajikita zaido kujenga nyumba za walimu.
Samia aliongeza kuwa serikali imeanzisha shule ya ufundi stadi ya Jakaya Kikwete iliyopo Kata ya Nangaro ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 70. Alibainisha kuwa ujenzi huo utakamilika kuwezesha vijana wapate ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa. “Hiyo ndiyo CCM, hatusemi kutoka ndotoni. Tukisema tunatekeleza,” alisisitiza.
Akizungumzia umeme, Samia alisema vitongoji vilivyosalia kufikishiwa huduma hiyo wakandarasi wanaendelea na kazi ikiwa ni utekelezaji ajenda ya nishati safi. Alisema serikali inatambua mahitaji ya miundombinu ikiwemo ukarabati wa barabara hivyo aliwaahidi maboresho ya barabara zilizoainishwa katika ilani ya uchaguzi.
Alitaja barabara hizo ni Milola – Kiwawa na zingine ambazo zitajengwa kwa kiwango cha changarawe kuwezesha zipitike muda wote. “Tutajenga stendi ya maroli hapa Mchinga ambayo itapunguza msongamano na kuongeza fursa za biashara ndani ya eneo hilo. Aidha, mkitupa ridhaa kwa sasa tunatambua kuna uvamizi wa wanyamapori.
Samia alisisitiza serikali itaweka doria za kutosha ili kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu wasiende kuharaibu mazao ya wananchi. SOMA: Dk. Nchimbi aahidi kukarabati barabara 16 Kilolo
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Join this online home job right now and start making more than $500 every single day. It’s easy work—if you know how to use Facebook, then this job is for you. No boss watching over you, and you can work whenever you want from home. I made $18,632 last month by doing this just 2 hours a day after college. Curious to know more or join? Just visit this website for details.
COPY THIS →→→→ http://Www.Cashprofit7.site