Majaliwa:Rais Samia ni mama wa maendeleo

PEMBA : MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuthibitisha kuwa ni mama wa maendeleo kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kijamii na kiuchumi nchini.

Akihutubia wananchi wa Jimbo la Kojani, Pemba juzi, Majaliwa alisema Serikali ya Awamu ya Sita imefanikisha ujenzi wa vituo vya afya vyenye uwezo wa kutoa huduma zote za msingi, hali iliyopunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo. SOMA: Mradi wa gesi Kinyerezi–Chalinze kujengwa

“Kwa sasa wananchi hawaendi umbali mrefu kupata huduma za afya, wataalamu wa afya wameajiriwa,” alisema. Alibainisha kuwa Samia ametekeleza pia maono yake ya kumtua mama ndoo kichwani kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa, ya kati na midogo ya maji, sambamba na kuvutia wawekezaji waliowekeza katika miradi mikubwa iliyotoa ajira kwa Watanzania.

Majaliwa alisisitiza Samia ni mgombea pekee mwenye maono ya kuivusha Tanzania, akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Oktoba 29, mwaka huu. Majaliwa alimpongeza mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa kuifungua Zanzibar kiuchumi na kugusa sekta mbalimbali za kijamii. “Uongozi wa Dk Mwinyi umegusa kila sekta ikiwemo miundombinu, elimu, afya, maji, michezo na huduma nyingine. Ni Daktari wa Maendeleo, nendeni mkamjazie kura,” alisema.

Aidha, Majaliwa alimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kojani, Hamad Chande akimtaja kuwa ni mtendaji, mzalendo na mchapakazi. “Ninamfahamu Chande. Ndiyo maana aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha. Mchagueni ili aendelee kuwaletea maendeleo,” alisema.

Kwa upande wake, Chande aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kumpa ridhaa ya kuendelea kuwa mbunge wao, akiahidi kusimamia kikamilifu shughuli za maendeleo.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button