CCM yaendeleza kampeni Longido

ARUSHA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Longido mkoani Arusha kimeendelea na kampeni zake za kuwanadi wagombea wake wa nafasi ya Ubunge na Udiwani na kumwombea kura Mgombea Urais wa Chama hicho, Dk Samia Suluhu Hassan ili aweze kupata kura za kishindo katika Jimbo lenye wakazi wengi wa jamii ya kifugaji ya Kimasai.
Katibu wa Mwenezi wa CCM, Wilaya ya Longido,Solomoni Lekui alisema hayo katika kata za Namanga, Gelai Lumbwa, Gelai Meirugoi na Longido katika mikutano ya hadhara ya kampeni na mwitikio wa wananchi wa kata hizo ni mkubwa na wako tayari kumpa kura Rais Samia, mbunge na kura za ndio kwa madiwani wote wa kata 20 za Jimbo hilo.
‘’Tumepania kuongoza kura za Rais Jimbo la Longido Kitaifa kwani Kimkoa hawana mpinzania kwani wananchi wa Longido wameahidi kujitoa na rekodi iliyowekwa mwaka 2020 Kimkoa itavunjwa kwa asilimia mia moja’’alisema Lekui.
Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido, Dk Steven Kiruswa aliwaomba wananchi wa Jimbo hilo vijana,wanawake na wazee kumpa kura za kishindo Rais na yeye na madiwani kwani serikali ya CCM imefanya mambo makubwa katika jimbo hilo hususani maji,elimu,afya na miundombinu na fadhila pekee kwa Rais ni kumpa kura za kutosha.
Dk Kiruswa alisema na kuwataka wananchi wa Longido ifikapo octoba 29 mwaka huu wawahi mapema katika vituo vya kupiga kura ili kutimiza wajibu wa kupiga kura na kumchagua mgombea bora ili aweze kuleta maendelea katika jimbo hilo na nchi na sio wengine ni wagombea wote wa chama cha mapinduzi ngazi ya urais, ubunge na udiwani.
Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido, Papa Nakuta amesema Rais Samia ni mgombea pekee mwenye sifa za kuliongoz anchi kuliko wagombea wote wa nafasi hiyo waliojitokeza kuwania nafasi hiyo na kuwataka wana Longido kutofanya makosa ya kujaza kura za kishindo kwa samia.
Nakuta alisema hayo katika kata ya Namanga na Longido yenye wakazi wengi mchanganyiko na kusema hakuna Samia katika Jimbo la Longido amefanya makubwa na fadhila ni kumpa kura za kishindo ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
‘’Nawaomba mmpe kura za kishindo Samia na wagombea ubunge na udiwani kwani wote washirikiane kuleta maendeleo Longido kwa maslahi ya wote na sio wagombea wengine,’’alisema Nakuta.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com