DC Arusha Mjini aipongeza taasisi kuitangaza miradi

MKUU wa Wialaya ya Arusha, Joseph Mkude ameipongeza taasisi ya Nasimama na Mama Tanzania (TNMT) kwa kujitoa na kuwa mstari wa mbele katika kuitangaza miradi ya maendeleo inayofanywa na iliyofanywa na serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkude alisema hayo wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo katika tukio lililofanyika katika viwanja vya jengo la Azimio la Arusha na kusema kuwa uamuzi wa Taasisi hiyo unapaswa kupongezwa kwa kuwa kuna baadhi ya watu wanadiriki kusema kuwa serikali ya Rais Samia haijafanya chochote kitu ambacho sio kweli.

Alisema ni wakati wa vikundi na taasisi nyingine kuiga mfano wa Taasisi ya Nasimama na Mama kwa kuizunhumzia serikali vizuri hususani katika miradi ya maendeleo midogo kwa mikubwa ambayo serikali imeofanya ili kusiwe na upotoshaji kwa jamii kuwa serikali haijafanya kitu.

Mkuu huyo pia ameipongeza taasisi kwa kutenga kiasi cha Sh milioni 150 kwa ajili ya mikopo kwa vijana na wanawake katika Kata 15 ndani ya Jiji la Arusha kwa ajili ya miradi ya ujasiliamali na kusema kuwa ni mwanzo mzuri wenye kuinga serikali katika kupambana na ajira ambazo hazitoshi hivyo kuwaelekeza rika hiyo kujikita katika kujitegemea.

Mkude alisema mwanzo wa taasisi hiyo unatoa mwanga na amewaomba viongozi kujitoa kwa hali na mali katika majukumu waliyoanzisha ili kuijengea sifa taasisi kuendelea kuaminika kwa jamii na serikali ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele kuizungumzia serikali katika kila jambo jema kwa maslahi ya nchi.

Naye, Mwenyekiti wa TNMT Kanda ya Kaskazini, Monica Suleiman amesema kuwa lengo la taasisi hiyo iliyokuwa katika Mikoa Arusha,Kilimanjaro,Tanga na Manyara ni kuielezea kwa kina miradi na kazi zinazofanywa na serikali ili jamii ielewe kwa maslahi ya nchi kwa ujumla.

Alisema pamoja na hilo pia imejikita katika kuwakomboa vijana na wanawake kwa kutoa mikopo bila riba na kwa kuanzia wataanza kutoa kwa kata 15 za Jiji la Arusha kwa kila kikundi kupewa shilingi milioni 10 na kila kikundi kinatakiwa kuwa na vijana ama wanawake wasiozidi kumi watakaotambulika na viongozi wa serikali ngazi ya kata.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa TNMT imejipanga kuhakikisha inawakomboa vijana na wanawake kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa mtaji wa kuanzisha miradi ya maendeleo kama mradi wa ufugaji na kilimo na kuacha kutegemea ajira serikali ambazo ni finyu.

Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa kabla ya kutoa fedha kwa vikundi hivyo watawawezesha vijana na wanawake kupata elimu ya mradi ili watakapoanzisha mradi wawe na uelewa mpana ikiwa ni njia mojawapo ya kutaka mradi huo uwe endelevu na sio.

Naye Muasisi wa Taasisi hiyo Nchini Ibrahimu Mwakabwanga alisema kuwa taasisi hiyo iko katika Mikoa zaidi ya mitano hapa nchini na malengo ni hayo hayo na kusema kuwa lengo ni kufumgua katika Mikoa yote nchini.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button