Mwinyi : Barabara za zege kujengwa Tumbatu

KASKAZINI UNGUJA : MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali katika awamu ijayo inatarajia kujenga barabara za zege katika kisiwa chote cha Tumbatu, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wanachama wa CCM na wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uvivini, Tumbatu, ambapo alisema tayari serikali imekabidhi kazi hiyo kwa mkandarasi na vifaa vimeanza kuagizwa kwa ajili ya kuanza ujenzi huo.
Amesema hatua hiyo inalenga kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa miundombinu bora ya barabara kisiwani humo, jambo ambalo litachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Tumbatu. SOMA: Samia azindua boti za bil 4/- za wavuvi Tanga
Aidha, Dk. Mwinyi alisema serikali pia imepanga kujenga gati jipya ili kurahisisha usafiri wa kuingia na kutoka kisiwani humo. Vilevile, alibainisha kuwa serikali inaendelea na mradi mkubwa wa maji unaohusisha kulazwa kwa bomba kubwa baharini ili kusambaza maji safi kwa wakazi wa Tumbatu katika kipindi kifupi kijacho.
Katika sekta ya uvuvi, Dk. Mwinyi alisema serikali itaendelea kuwawezesha wavuvi kwa kuwapatia boti za kisasa na vifaa vya uvuvi ili waweze kuvua katika maeneo ya bahari kuu. Pia aliahidi kuboresha huduma za afya na elimu kwa kuajiri madaktari, wauguzi na walimu wapya, sambamba na kuipatia vifaa vya kisasa hospitali ya wilaya inayojengwa kisiwani humo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Muhammed Said Dimwa, alisema uongozi wa Dk. Mwinyi katika miaka mitano iliyopita umeleta maendeleo makubwa Zanzibar na hasa katika Kisiwa cha Tumbatu, hivyo akawataka wananchi kumpa tena ridhaa ya kuongoza pamoja na wagombea wengine wa CCM ili kuendeleza mafanikio hayo.
Join this online home job right now and start making more than $500 every single day. It’s easy work—if you know how to use Facebook, then this job is for you. No boss watching over you, and you can work whenever you want from home. I made $18,632 last month by doing this just 2 hours a day after college. Curious to know more or join? Just visit this website for details.
Open This→→→→ http://Www.Work99.Site