Majaliwa kufungua Wiki ya Vijana Kitaifa Mbeya

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2025, Oktoba 10 yanayofanyika kwenye viwanja vya Uhindini jijini Mbeya kuanzia Oktoba 8-14.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete amebainisha hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Ridhiwani amesema maadhimisho ya Wiki ya Vijana 2025 yatakwenda sambamba na Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba 14 ambapo ni siku ya mapumziko.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya.(Picha na Joachim Nyambo)

Amesema lengo la Maadhimisho ya Wiki ya Vijana kitaifa ni kuwakutanisha vijana kutoka pande zote nchini na kuwawezesha kubadilishana uzoefu na ukweli wa fursa mpya za nyanja kiuchumi na kijamii.

Amebainisha kuwa miongoni mwa shughuli zitakazofanyika wakati wa maadhimisho hayo yakiendelea kuwa ni pamoja na maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali, wabunifu, makongamano na kazi za kujitolea na kusaidia jamii.

SOMA: Taasisi yaenzi miaka 101 ya Nyerere

Waziri huyo amesema kwa upande wa kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru baada ya kukimbizwa katika Halmashauri zote za Mikoa 31 iliyopo nchini sherehe za uzimaji zitafanyika ndani ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.

Kwa upande wa kumbukizi ya miaka 26 ya Baba wa Taifa amesema kabla ya kuunganishwa na shughuli ya uzimaji Mwenge wa Uhuru ndani ya Uwanja wa Sokoine itatanguliwa na Ibada ya Misa maalumu ya Kitaifa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwanjelwa jijini Mbeya.

Amesema pia taarifa kamili ya kazi zilizofanywa na Mwenge wa Uhuru wakati wa mbio zake mwaka huu itatolewa katika Uwanja wa Sokoine mbele ya mgeni rasmi, Rais Samia Suluh Hassan.

Waziri huyo amewasihi wakazi wa mkoa wa Mbeya na maeneo ya jirani kufika kwa wingi kwenye maeneo yote yatakayohusisha matukio hayo ya kitaifa ili kuungana na kuonesha ukarimu kwa wageni watakaofika mkoani humo kwa ajili ya ushiriki.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi jijini Mbeya wametaja ujio wa matukio hayo ya kitaifa kuwa fursa inayoweza kuwanufaisha iwapo watajiweka tayari hususani kwenye shughuli za kiuchumi hasa uuzaji bidhaa za aina mbalimbali zikiwemo vyakula na vinywaji.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button