NCCR Mageuzi yahimiza amani, yahadharisha vurugu

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi), Haji Ambari Khamis amesema wananchi wakimchagua, atailinda amani ya nchi.
Khamis alitoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma juzi.
Alisema serikali yake itadumisha na kuimarisha amani iliyodumu kwa muda mrefu nchini, kwa kuwa ni msingi wa maendeleo endelevu.
Khamis alisema amani ni sera kuu ya chama hicho na akatoa mwito kwa Watanzania wakatae majaribio yoyote ya kuchochea machafuko.
“Sera yetu katika NCCR-Mageuzi ni amani. Msikubali wala kushawishika na watu wanaotaka kuvuruga utulivu wa nchi yetu. Watu wa aina hiyo hawalitakii mema taifa hili,” alisema.
Kwa mujibu Khamis katika nchi ambazo zimepoteza amani, wanawake, watoto, wazee na vijana wanaumia zaidi.
“Katika vita, watu huishi kwenye mahandaki kwa wiki nzima, wakitegemea chakula na maji kidogo. Ni bora mataifa yakatofautiana kwa hoja kuliko kuingia katika vita vya ndani,” alisema.
Khamis aliwasihi Watanzania wakatae lugha za chuki na kuulinda umoja wa kitaifa.
Pia, alitoa mwito kwa wananchi wamheshimu rais na wajiepushe na matusi, akibainisha kuwa mkuu wa nchi anawakilisha wananchi waliomchagua.
“Unapomtukana rais, unawatukana Watanzania wenyewe. Tusikubali kuingizwa kwenye chuki na migogoro, kwa sababu hali hizo huanza kidogokidogo na hatimaye huangamiza taifa,” alisema Khamis.
Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Dk Evaline Munisi alieleza dira ya chama hicho kuhusu uchumi, akiahidi kuanzisha viwanda katika kila kata kulingana na mazao ya kilimo ya maeneo husika, ili kuongeza thamani ya mazao hayo.
Dk Munisi alisema katika serikali wanayopendekeza, bei za bidhaa zitaamuliwa na wananchi wenyewe badala ya kuwekewa na serikali, ili kuhakikisha ushiriki wa haki katika soko.
Katika kusaidia upanuzi wa viwanda hivyo vidogo, alibainisha mipango ya kuanzisha vituo vya mafunzo ya ufundi stadi katika kila kata, kulingana na mahitaji ya eneo husika.
“Bahi kwa sasa ina kituo kimoja tu cha mafunzo ya ufundi, ambacho hakitoshi. Tunataka kuwapatia vijana ujuzi wa vitendo kwa kuanzisha vituo zaidi vitakavyofundisha ubunifu, useremala, ushonaji, ujenzi na fani nyingine mbalimbali” alisema Dk Munisi.
Alisema uanzishaji wa viwanda vidogo utaongeza ajira kwa wanawake, vijana na wanaume, hivyo kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika Wilaya ya Bahi na Mkoa wa Dodoma kwa ujumla.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com