Wananchi Babati wapata huduma za afya ya akili

MANYARA: HOSPITALI ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe imeadhimisha Siku ya Afya ya Akili Duniani mwaka 2025 kwa kuandaa kambi maalumu ya matibabu, ushauri na mafunzo ya afya ya akili katika Wilaya ya Babati, mkoani Manyara.

Hatua hiyo inalenga kutoa huduma bure kwa wananchi na kuelimisha watoa huduma kuhusu afya ya akili wakati wa majanga na dharura.

‎Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Upatikanaji wa huduma ya afya ya akili wakati wa majanga na dharura,” ikilenga kuhamasisha jamii na taasisi za afya kuwekeza zaidi katika huduma za afya ya akili, hasa kwa maeneo yaliyoathirika na majanga ya asili kama vile mafuriko, maporomoko ya ardhi na matukio mengine yanayochangia athari za kihisia na kiakili kwa wananchi.

‎Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya  Motel Papaa, vilivyoko wilaya ya Babati tarehe 10 Oktoba 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dk. Paul Lawala, amesema maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika mkoani Manyara kutokana na historia ya majanga yaliyotokea hivi karibuni katika Wilaya ya Hanang, ambayo yaliacha athari kubwa kwa afya ya akili ya wakazi wake.

‎“Mkoa huu umekumbwa na matukio kadhaa ya majanga na dharura, ikiwemo maafa ya Hanang. Athari kama hizi huacha majeraha makubwa ya kiakili, hivyo tunahakikisha jamii inapata elimu, huduma na msaada wa kitaalamu wa afya ya akili,” amesema Dk. Lawala.

‎Ameongeza kuwa lengo la kuweka kambi ya matibabu Babati ni kutokana na ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia, ulevi uliokithiri na matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wananchi wa mkoa huo, hali inayochangia ongezeko la wagonjwa wa afya ya akili wanaohitaji huduma maalumu.

‎Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, amepongeza Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kwa kuandaa kambi hiyo muhimu ya huduma na elimu ya afya ya akili.

‎Akifungua rasmi amesema maadhimisho hayo yamekuja wakati muafaka, hasa baada ya mkoa huo kukumbwa na maafa ya Hanang ambayo yaliathiri kwa kiasi kikubwa afya ya kiakili ya wakazi.

‎“Kaulimbiu ya mwaka huu inagusisha moja kwa moja maisha yetu kama Watanzania. Baada ya maafa ya Hanang, wananchi wengi walipoteza wapendwa, makazi na mali, hali iliyoathiri afya yao ya akili. Hivyo, ujio wa Hospitali ya Mirembe ni faraja kwa wananchi wa Manyara,” amesema.

‎“Zamani tulizoea kuona wanawake wakiwa wahanga wa ukatili wa kijinsia, lakini sasa hali imebadilika. Wanaume nao wameanza kuwa wahanga, na tayari kuna chama cha wanaume wanaopitia ukatili kutoka kwa wenza wao. Hii inaonyesha umuhimu wa elimu ya afya ya akili kwa jamii nzima bila kujali jinsia,” amesisitiza Mkuu wa Mkoa.

‎Timu iliyofika Manyara inajumuisha madaktari bingwa wabobezi wa afya ya akili, wanasaikolojia, wauguzi, wafamasia, wataalamu wa ustawi wa jamii na tiba kazi, ambao watakuwa Babati kwa siku tatu kutoa huduma bure za matibabu, ushauri nasihi na mafunzo kwa watoa huduma kutoka sekta mbalimbali.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button