Serikali yapongezwa kumuenzi Baba wa Taifa

SERIKALI imepongezwa kwa kusimamia amani, utulivu na umoja wa kitaifa miaka 26 tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipofariki dunia mwaka 1999.

Viongozi wastaafu na wahadhiri wamelieleza gazeti HabariLEO ilikuwa ndoto ya Nyerere kujenga taifa lenye umoja na mshikamano, likiwa na amani na utulivu.

Mwanasiasa mkongwe, Paul Kimiti amesema serikali inastahili pongezi kwa namna ilivyoenzi maono na ndoto za Nyerere kwa kulifanya taifa kuwa tulivu, huku Watanzania wakiendelea kufanya kazi kwa ajili ya uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Ameishauri serikali kuzidisha usikivu kwa wananchi kwa sababu Nyerere alikuwa akiwasikiliza wananchi wote mpaka wa mtaani, ili kujua hisia zao na malalamiko yao ili kuyafanyia kazi.

Ameongeza: “Baba wa Taifa alihusia serikali isiwapuuze wananchi. Inatakiwa kuwasikiliza maoni na malalamiko yao na kuchukua hatua ya kurekebisha pale ilipojisahau, mpaka wananchi wakalalamika.”

Kwa upande wake, Mwanahistoria nguli wa Tanzania, Mohamed Said katika mazungumzo na gazeti hilo amesema Nyerere katika kusisitiza umuhimu wa amani na utulivu, aliwahusia Watanzania wasichoshwe na amani na kutamani vurugu.

Amesema kutokana na maendeleo ya kisiasa katika mataifa mengine duniani kutawaliwa na vurugu za wenyewe kwa wenyewe,

Nyerere aliamua kutoa tahadhari kuwa Watanzania muda wote wamekuwa katika kisiwa cha amani na utulivu, hivyo isitokee siku moja wakatamani kuipoteza.

“Mwalimu alifahamu kuwa kwa misingi waliyoijenga, kuipoteza amani ingekuwa vigumu sana kuipata tena. Ndio maana akahusia Watanzania wasichoke amani wakatamani vita,” ameongeza.

Amesema tangu limetolewa angalizo hilo, serikali zote zilizofuata zilijitahidi kulinda na kuimarisha amani na mshikamano kuanzia Serikali ya Awamu ya Pili, Tatu, Nne, Tano na hii ya Awamu ya Sita.

Naye mwanasiasa wa zamani, Anna Abdalla amesema serikali zote zilizofuata baada ya Nyerere kuaga dunia zilijitahidi kuendeleza amani na umoja wa kitaifa kuanzia Rais Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli na sasa Samia Suluhu Hassan.

Amesema kila kiongozi alijitahidi kuendeleza ndoto ya Nyerere kwa kutunza amani na kuendeleza mapambano dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi.

Amesema anaamini maeneo na changamoto chache zilizobaki zitaendelea kushughulikiwa, kwa sababu hakuna serikali duniani ambayo ilimaliza changamoto zake zote kwa wakati mmoja.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na Utawala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Richard Mbunda amesema serikali kwa kiasi kikubwa imejitahidi kulinda na kudumisha misingi ya amani na utulivu kama malengo ya Nyerere yalivyokuwa.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

    1. Make money while staying at home and working online. I just received $23,783 for my work last month, and I was doing this part-time. This year, I plan to earn even more, and I believe you can also make extra cash from this job. To join right now, follow the details on this website.

      Open This… http://Www.Work99.Site

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button