UNCDF waongoza mjadala Dira 2050

MFUKO wa Mitaji ya Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF), kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na wadau mbalimbali wa maendeleo, umekutana katika mkutano maalum wa kujadili mabadiliko ya mazingira ya ufadhili na mwelekeo wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.
Mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam, uliwakutanisha viongozi wa serikali, mabalozi, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi na asasi za kiraia, ambapo wadau walijadiliana kwa kina kuhusu njia za kutafsiri malengo ya kitaifa kuwa matokeo halisi kwa wananchi.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda, alisema dunia kwa sasa inatumia zaidi ya dola trilioni 2.7 kila mwaka kwa masuala ya usalama, wakati kiasi kidogo cha fedha hiyo kinatosha kumaliza njaa na kutoa huduma bora za afya kwa wote duniani.
“Huu ni wakati wa kuchukua hatua kwa pamoja na kuendana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2050. Kupitia mifumo mipya ya ufadhili kama vile matumizi ya rasilimali za ndani, ushirikishwaji wa sekta binafsi, uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, na matumizi ya hati fungani za kijani na za manispaa, tunaweza kuleta maendeleo jumuishi na yanayostahimili mabadiliko ya tabianchi,” alisema Balozi Kaganda.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa, Dk Fred Msemwa, alisema dira hiyo inalenga kuiweka sekta binafsi kama injini ya uchumi, huku serikali ikibaki kuwa mwezeshaji na mtoa mazingira rafiki kwa wawekezaji.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Susan Nyamondo, alisema mafunzo yaliyopatikana kupitia mkutano huo yatasaidia kuoanisha vipaumbele vya serikali na mikakati ya washirika wa maendeleo, akitoa mfano wa mafanikio ya hati fungani ya kijani ya Tanga UWASA kama mfano bora wa ubunifu wa kifedha kwa maendeleo endelevu.
Katika mijadala ya wataalamu na wadau, John Viner kutoka Ubalozi wa Sweden alisema kuwa mwelekeo mpya wa misaada ya maendeleo wa Sweden umejikita zaidi kwenye matumizi bora ya rasilimali na uwekaji wa dhamana ili kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi. SOMA: TCCIA, EABC kutoa mitaji kwa vijana nchini
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Gatsby Africa, Samwel Kilua, alisisitiza umuhimu wa washirika wa maendeleo kuelewa mazingira halisi ya Tanzania na kuongeza thamani kwenye miradi iliyopo badala ya kufanya kazi kwa kujitenga.
Mkutano huo pia uliangazia mafanikio ya UNCDF nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kusaidia biashara ndogo na za kati kupata huduma za kifedha, kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na uwekezaji kwenye mifumo ya chakula kupitia kilimo.
Pia, ziliwasilishwa mifumo ya kiubunifu ya ufadhili kama vile hati fungani za kijani, uwekezaji unaozingatia viwango (standards-aligned investments) na mpango wa LoCAL, unaolenga kusaidia miji midogo kukabiliana na athari za tabianchi. Washiriki wa mkutano huo walihimizwa kuendeleza ubunifu, kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi, na kupanua miradi iliyokwisha onyesha mafanikio ili kuleta maendeleo jumuishi na endelevu kwa Watanzania.
Make money while staying at home and working online. I just received $23,783 for my work last month, and I was doing this part-time. This year, I plan to earn even more, and I believe you can also make extra cash from this job. To join right now, follow the details on this website.
Open This… http://Www.Work99.Site
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website
COPY HERE→→ http://Www.Work43.comᴵᴵᴵ