‘Mwana FA’ awaita mashabiki “Road to BAL’

DAR ES SALAAM:NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA), amewataka mashabiki wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano ya kimataifa ya mpira wa kikapu “Road to BAL”, yatakayofanyika kesho (Ijumaa) katika Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya raundi ya awali yatashirikisha timu ya Dar City kutoka Tanzania, pamoja na timu kutoka Uganda na Visiwa vya Comoro. Timu mbili zitakazoongoza zitasonga mbele hatua ya 16 bora, itakayochezwa nchini Kenya au Afrika Kusini, ambako timu nne bora zaidi zitafuzu hatua ya robo fainali.
“Mashindano haya si jambo dogo kwa mchezo wa kikapu. Ni fursa kwa Watanzania kujionea mashindano ya kimataifa yakichezwa hapa nyumbani,” amesema Mwinjuma.
Ameongeza kuwa serikali inafarijika kuona maendeleo ya mchezo huo nchini, huku akipongeza klabu ya Dar City kwa maandalizi bora na ushiriki wake katika mashindano ya kimataifa.
“Mmehakikisha mchezaji wa Kitanzania anakuwa nahodha wa timu. Nawaomba mashabiki wa michezo waje kwa wingi kushuhudia burudani hii ya kikapu,” alisisitiza Mwinjuma.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameipongeza Dar City kwa kuonyesha mwelekeo wa kimataifa kupitia uwepo wa Kocha Pabi Gueye kutoka Senegal.
“Tumezoea kuona timu zetu zikiwa na makocha wazawa, lakini sasa tunashuhudia timu yenye taswira ya kimataifa. Ni ishara nzuri kwa maendeleo ya kikapu nchini,” alisema Chalamila.
Aliongeza kuwa mashindano hayo ni fursa kwa wananchi kushuhudia michezo ya kiwango cha juu na kuimarisha umoja wa kitaifa kupitia michezo.
Kwa upande wake, Nahodha wa Dar City, Hasheem Thabit, alisema kikosi chake kipo katika maandalizi ya mwisho na kipo tayari kuonesha uwezo mkubwa.
“Tupo vizuri. Tunaomba Watanzania waje kutusapoti. Kikapu bado kinakabiliwa na changamoto za udhamini, lakini tumeendelea kupambana,” amesema Thabit.
Amefafanua kuwa yeye na Musa Mzenji wamekuwa mstari wa mbele kuwekeza katika timu hiyo, huku akihamasisha wazazi kuwahimiza watoto kushiriki michezo kwani ni ajira, maisha, na malezi bora kwa vijana.
Naye Kocha wa Dar City, Pabi Gueye, alisema amefurahia mazingira mazuri ya Tanzania na kuahidi burudani ya hali ya juu kesho.
“Nimefurahia kuwa Tanzania. Mazingira ni mazuri, timu ipo vizuri, na naamini mashabiki watafurahia burudani tutakayotoa kesho,” amesema Gueye.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali wa kikapu kutoka Marekani na mataifa mengine, wakiongozwa na Hasheem Thabit, mchezaji wa kimataifa wa Tanzania.
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com