Wenye ulemavu Moro wapo tayari kupiga kura

MOROGORO: WATU wenye Ulemavu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura wapo tayari kushiriki upigaji kura Oktoba 29, mwaka huu kutokana na kupatiwa elimu ya mpiga kura na Taasisi zisizo za Kiserikali ambazo zimepewa kibari cha kutoa elimu hiyo na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu mkoa wa Morogoro wamesema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa kizugumzia namna watakavyoshiriki kwenye upigaji kura uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mweka Hazina wa Chama cha Watu Wenye Ualbino( TAS), Mkoa wa Morogoro, Aziza Dilunga, amesema viongozi na wanachama wamepatiwa elimu ya namna ya kutumia haki ya msingi ya kikatiba ya mpiga kura kuchagua viongozi wanaowafaa wao na taifa kwa ujumla.
“Mpaka sasa hivi mtu mwenye ulemavu anayo haki ya kupiga kura pia haki ya kuchagua na kuchaguliwa,”amesema Aziza.
Mbali na hayo amesema watu wenye ualbino wanachangamoto za uoni hafifu, hivyo aliomba maandishi yawe makubwa na kwamba chama kinajivunia kwa sababu kina watu ambao wanajitambua na kujielewa katika suala zima ya upigaji kura.
Naye Katibu wa Chama cha Watu wenye Ulemavu wa Viziwi ( CHAVITA), Wilaya ya Morogoro, Christopher Mkumbi amesema wanachama wamejiandikisha kupiga kura kwa sababu kutakuwa na karatasi za kupigia kura ambazo zina maandishi ya nukta ndundu.
“ Uchaguzi mkuu wa mwaka huu umekuwa na maboresho makubwa kwetu sisi wenye ulemavu wa kutoona ,tofauti na miaka mingine kwa kuwepo karatasi wenye nukta nundu na kumwezesha kushiriki kupiga kura bila kupigiwa na mtu” amesema Makumbi.
Amesema changamoto anayoiona ni kwa wale ambao wameupata ulemavu ukubwani na hawana elimu ya kusoma maandishi nukta nundu, ingawa na wao wanaweza kwenda vituoni na wasaidizi wao wanaoaamini.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha aWatu Wenye Ulemavu wa Viungo ( CHAWATA), wilaya ya Morogoro. Ramadhan Feruzi amesema kundi hilo limejipanga vizuri kushiriki uchaguzi.
Feruzi amesema walishapatiwa elimu ya mpiga kura , hivyo wanaowajibu kikatiba kushiriki kupiga kura za kuwachangua viongozi wanawaona wanawafaa wao wenyewe na Taifa.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini, Elizabeth Ngobei, amesema wamejipanga vizuri kuhusiana na suala nzima la uchaguzi wa Rais, Mbunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29 , 2025.
“ Kwa wale wenzetu ambao hawaoni kutakuwa na matumizi ya nukta nundu kwa ambao wanaweza kuzitumia kutakuwa na karatasi hizo na wataweza kutumia ili waweze kupiga kura vizuri” amesema Ngobei .
“ Pia tutatumia vitotori ambavyo ni rafiki kwa watu wote kwa ambao sio walemavu na wenye ulemavu kwa maana ya kwamba yule wenye ulemavu ataweza kukigeuza kitotori kile na yeye akaweza kuwa vizuri kwa ajili ya kuweza kupiga kura yake akiwa katika mazingira mazuri na salama” amesema Ngobei .
Amesema kwa wale ambao watakuwa na mahitaji maalum kwa mfano wenye ulemavu ,wanawake wajawazito, wazee na watakaokuja na watoto wadogo katika vituo vya kupigia kura wanapewa kipaumbele cha kuweza kupiga kura kwa haraka na kuweza kurudi nyumbani.
Morning UDIWANI, I am so bored we can chat about sexy things, text me here: https://hookupdate.lol/?photos&s=Beauty139z
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Morning UBUNGE, I am so bored we can chat about sexy things, text me here: https://hookupdate.lol/?photos&s=Beauty139z
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Morning URAIS, I am so bored we can chat about sexy things, text me here: https://hookupdate.lol/?photos&s=Beauty139z
Morning Waziri Mkuu, I am so bored we can chat about sexy things, text me here: https://hookupdate.lol/?photos&s=Beauty139z
Morning Uspika, I am so bored we can chat about sexy things, text me here: https://hookupdate.lol/?photos&s=Beauty139z