Serikali bega kwa bega na wafugaji Ngorongoro

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeendelea kuzijali jamii za kifugaji, hasa katika maeneo ya pembezoni kama Wilaya ya  Ngorongoro mkoani Arusha kwa kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi hao zinapatiwa suluhisho la kudumu.

Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM(NEC), Namelok Sokoine na kusema kuwa serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imechukua hatua mbalimbali za kutatua migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kujenga umoja na maendeleo kwa wote bila kubagua.

Namelok ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni wa kusaka kura za Rais wabunge na madiwani wa CCM katika kata ya Ngaresero katika jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha.

Kwa upande wake, Yanick Ndoinyo, mgombea ubunge pekee wa jimbo la Ngorongoro kupitia CCM, amezitaka jamii za kifugaji kutumia kura zao kama silaha ya maendeleo, akisisitiza umuhimu wa ushiriki mkubwa katika uchaguzi

Naye Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, amewataka viongozi wa serikali za mitaa kusaidia wananchi wa maeneo ya mbali kufika vituoni siku ya kupiga kura, akisisitiza kuwa kila mtanzania anapaswa kupata haki ya kushiriki katika maamuzi ya mustakabali wa nchi yake.

Wananchi wa jamii za kifugaji Ngorongoro wamesema wako tayari kumpa Rais Samia Suluhu Hassan ushindi wa kishindo kama ishara ya kuthamini jitihada za serikali ya CCM katika kuboresha maisha yao ikiwemo huduma za kijamii, miundombinu na upatikanaji wa ardhi salama kwa ajili ya mifugo yao.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button