Vituo vya nishati vyachochea maendeleo ya uchumi

DAR ES SALAAM :ZAIDI ya vituo 10 vya huduma jumuishi vikiwemo vya nishati vimejengwa nchini kwa kipindi cha miezi kumi huku vituo hivyo vikitajwa kusaidia kuchochea maendeleo pamoja na kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.
Akizungunza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kituo jumuishi cha huduma za nishati cha Puma Mbezi Beach Mkurugenzi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Fatmah Abdallah amesema vituo hivyo vimejengwa sehemu mbalimbali nchini ambapo vimesaidia kusogeza huduma za nishati hasa mafuta na gesi hivyo kuwasaidia wananchi.
Kwa upande wake Benedict Ndunguru Mkuu Kitengo cha biashara Puma amesema hatua ya uzinduzi wa kituo hicho cha mbezi beach ni katika kuunga mkono jitihada za serikali za kusogeza huduma za nishati karibu na wananchi ili kupunguza safari ndefu ya kufuata huduma za nishati mbali na maeneo yao.
Nao baadhi ya wananchi wanaotumia huduma za nishati Gifta Mlacha na Asma Abdala wameshukuru kutokana na huduma kusogezwa huku wakitaka kampuni nyingine nazo kuiga mfano wa kusogeza huduma kwa jamii.



